Chama cha
Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kimepokea kwa mstuko mkubwa taarifa za kifo cha
Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Bi. Christina Kibikia liyeuawa kwa
kupigwa risasi na watu wasiyojulikana.
Taarifa
iliyotolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo
CPA Amos Makalla imesema kuwa marehemu alikuwa anajindaa kuhudhuria Semina elekezi
kwa Makatibu Mjini Dodoma kesho.
CPA Makalla
amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia, ndugu, viongozi na wanachama
wa CCM mkoa wa Iringa kufuatia kifo hicho cha ghafla na cha kikatili.
Amemalizia
kwa kusema kuwa, “Tunawaomba wanachama wetu wawe watulivu wakati vyombo vya dola
vikifuatilia na kuchunguza tukio hili, ili wahusika waweze kufikishwa katika vyombo
vya kisheria.”

0 Maoni