Kichaa cha mbwa huathiri zaidi mabara ya Asia na Afrika

  

Kichaa cha mbwa ni tatizo kubwa la afya katika nchi zaidi ya 150, hususan barani Asia na Afrika, Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa leo imesema. 

WHO imesema ugonjwa huu wa virusi unasababisha maafa ya maelfu ya vifo kila mwaka, ambapo asilimia ya wahathiriwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka 15. 

Shirika hilo limesema mara tu virusi vinapofikia ubongo na uti wa mgongo na dalili zake huanza kuonekana, ugonjwa huu daima ni hatari kwa maisha. 

“Hivyo, chanjo ni muhimu sana. Ni muhimu kutafuta matibabu mara moja baada ya kuumwa na mbwa,” imesema taarifa hiyo ya WHO. 

Asilimia 99% ya matukio ya kichaa cha mbwa kwa binadamu yanatokana na kuumwa na mbwa au kuchubuliwa. Unaweza kuzuia kwa kuchanja mbwa na kuepuka kuumwa, imemalizia taarifa hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni