Ureno kuzindua sarafu ya CR7 kwa heshima ya Ronaldo

 

Nchi ya Ureno inatarajia kuzindua sarafu ya Euro 7 ya Christiano Ronaldo, kama heshima na shukrani kwake kutokana na mafanikio yake makubwa katika mchezo wa soka duniani.

Sarafu hiyo yenye picha ya mchezaji huyo mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora duniani (Ballon d'Or) imewekwa pia alama maarufu ya utambulisho wake ya CR7.

Sarafu pia ni kwa ajili ya kutambua mchango wake kwa timu yake ya taifa ambayo, nahodha huyo aliisaidia kutwaa Kombe la Mataifa ya Ulaya (EURO 2016).

Christiano Ronaldo, anaongoza orodha ya wafungaji bora katika timu ya taifa ya Ureno, akiwa amepachika kimiani mabao 131.

Hivi karibuni, nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 alifunga bao lake la 901 dhidi ya Scotland kwenye michuano ya UEFA Nations League.

Chapisha Maoni

0 Maoni