Harris na Trump watoana jasho dakika 90 za mdahalo

 

Kamala Harris na Donald Trump wamechuana vikali katika mdahalo wa dakika 90 huko Philadephia, ukiwa ni mdahalo wao wa kwanza wa kinyang’anyiro cha urais wa Marekani 2024.

Baada ya kupeana mikono, kwa mara ya kwanza kukutana, wagombea hao wa urais wa Marekani waliongelea sera zao kabla ya kuanza kushambuliana kwa maneno.

Harris alimponda Trump kwa kusema watu huondoka mapema kwenye mikutano yake kutokana na kuchoshwa, huku Trump akisema watu hawaendi kabisa kwenye mikutano ya Harris.

Trump pia alishambulia sera za uhamiaji na mipaka za Harris, huku Harris naye akimshutumu Trump kwa tukio la shambulizi la US Capitol la Januari 6.

Matokeo ya awali ya mdahalo huo yanaonyesha Harris kushinda, ingawa Trump amedai kuwa amepoteza vibaya mno.

Chapisha Maoni

0 Maoni