Polisi waungana duniani kudhibiti mtandao wa uhalifu wa Nigeria


Vikosi vya polisi duniani vimeunganisha nguvu na kufanya operesheni za mfululizo zinazolenga kuukabili moja ya mtandao uhalifu unaohofiwa wa Afrika Magharibi wa Black Axe.

Operesheni hiyo iliyopewa jina la Jackal III imehusisha maafisa wa polisi waliosheheni silaha wakivamia maeneo katika mataifa 21 kati ya Aprili na Julai 2024.

Zoezi hilo linaratibiwa na Shirika la Polisi la Kimataifa limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 300 wenye uhusiano na kundi la uhalifu wa mitandaoni la Black Axe pamoja na makundi mengine.

Interpol imesema operesheni hiyo ni pigo kubwa kwa mtandao huo wa uhalifu wa Nigeria, lakini imeonya kuwa mtandao wake wa kimataifa na teknolojia wanaoitumia inabaki kuwa ni tishio.

Chapisha Maoni

0 Maoni