Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuongeza
uadilifu na kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao sambamba na
kuongeza kasi katika utendaji kazi.
Mhe. Ndejembi namesema, suala la ardhi ni gumu na linahitaji
watumishi kuwa makini ambapo amesisitiza kuwa ni lazima watumishi wa sekta ya
ardhi watende haki huku wakizingatia kuwa kuna sheria, kanuni na miongozo
inayowaoongoza katika utendaji kazi.
Aidha, Mhe. Ndejembi amesema, yale yote mazuri yaliyofanywa
na mtangulizi wake ikiwemo Klinik za Ardhi atayaendendeleza kwa lengo la kuleta
ufanisi wa wizara.
‘’Sikuja kutengua torati, yote aliyoyaanzisha mtanguluzi
wangu ikiwemo klinik za ardhi zitaendelea na vile vile anayehisi jambo lake
limekwama ajitokeze na atahudumiwa,’’ amesema Mhe. Ndejembi.
Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo tarehe 26 Julai 2024 wakati
akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wizara ya Ardhi mkoa wa Dar es
Salaam mara baada ya kutoka kuapishwa kushika nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi
wake Mhe. Jerry Silaa.
Sambamba na hayo Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi ametaka kuimarishwa kwa mifumo ndani ya wizara ili migogoro ya ardhi
isiendelee kujitokeza.
Mhe. Ndejembi ameapishwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitokea Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu).
Na Munir Shemweta- WANMM
0 Maoni