Prof. Muhongo kushirikiana na wanavijiji kujenga sekondari mpya sita

 

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo ameridhia ombi la kushirikiana na wanavijiji wa jimbo lake kuanzisha miradi ya ujenzi wa sekondari mpya sita.

Hatua hiyo inafuatia wanavijiji hao kumuomba Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini washirikiane naye kuanza miradi yao ya ujenzi wa sekondari hizo mpya.

Mwamko wa elimu wa wanavijiji wa jimbo la Musoma Vijijini ambalo lina Kata 21 zenye vijiji 68, vitongoji 374 na sekondari 26 za kata na mbili za binafsi, umemgusa Mbunge wa Prof. Muhongo.

Ofisi ya mbunge huyo imesema, sekondari hizo mpya zitajengwa kwenye Kijiji cha Chitare, Kijiji cha Buanga, Kijiji cha Nyambono,  Kijiji cha Kataryo,  Kijiji cha Kiriba pamoja na ya Kijiji cha Mmahare.

Taarifa hiyo ya mbunge Prof. Muhongo imesema unjenzi wa sekondari hizo sita unatarajiwa kuanza Julai/Agosti 2024 kwa kutumia michango ya wanavijiji na viongozi wao. 

Aidha, jimbo hilo kuna Sekondari mpya tatu zinajengwa kwa fedha za Serikali Kuu na Wanavijiji kuchangia nguvukazi na nyingine tatu mpya zinajengwa kwa michango ya wanavijiji na viongozi wao.

Taarifa za shule za msingi, hususani ujenzi wa shule shikizi mpya, na vyumba vipya vya madarasa zitatolewa baadae, imesema taarifa hiyo ya Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini.

Chapisha Maoni

0 Maoni