Mtuhumiwa akiri kuhusika na mauaji ya wanawake 42 Kenya

 

Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanaume mmoja anayefahamika kama Jomaisi Khalisia (33) mkazi wa Mtaa wa Kayole Kaunti ya Nairobi ambaye wanadai amekiri kuwaua wanawake 42 tangu 2022, akiwemo mke wake.

Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja, amesema kijana huyo anatoka kaunti ya Vihiga na alikamatwa akiwa mafichoni, huku akisema tayari wamepata miili 9 na kuwataka waliowapoteza wapendwa wao kuripoti Polisi.

Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohamed Amin, amesema baada ya kumhoji, mtuhumiwa huyo amekiri kufanya mauaji hayo, na kwamba ameua zaidi ya wanawake 42 kati ya mwaka 2022 na tarehe 11 mwezi Julai mwaka 2024.

Maafisa wa upelelezi wamefanikiwa kupata kadi 24 za simu, simu nane na panga miongoni mwa vitu vingine ambavyo wanaamini mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia kutekeleza matukio hayo ya mauaji ya kinyama.

Chapisha Maoni

0 Maoni