Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan
Abbasi leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini India,
Mhe. Anisa Mbega kuhusu mikakati ya
kuutangaza zaidi utalii wa Tanzania nchini India.
Kikao hicho kimefanyika leo Julai 25,2024 katika Ofisi za
Ubalozi wa Tanzania nchini India.
“Tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan alipofanya Filamu ya Tanzania The Royal Tour pamoja na
juhudi za sekta binafsi na nyie Mabalozi nchi yetu imeendelea kupokea mafuriko
ya watalii lakini bado tunahitaji kuongeza mikakati zaidi hasa kwa nchi kama
India yenye watu takribani Bilioni 1.4 “alisema Dkt. Abbasi ambaye yupo jijini
Delhi kuhudhuria Mkutano wa Kamati ya Urithi wa Dunia ya UNESCO.
Amesema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa, bado soko la
watalii ni kubwa na kwamba linatakiwa kufikiwa kimkakati zaidi.
Kwa upande wake Balozi Anisa amesema kuwa India ni soko kubwa na hivyo Ubalozi pamoja na mikakati mbalimbali inayoendelea nayo ikiwemo kushiriki makongamano ya utalii katika miji ya India, amefurahishwa na ujio wa Katibu Mkuu wa sekta husika kwani utaimarisha mikakati iliyoanza kutekelezwa.
0 Maoni