Zoezi la 13 la Medani la Vikundi Vya Ulinzi, Usalama na
Taasisi za Kiraia vya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (FTX
Ushirikiano IMARA 2024) limefungwa rasmi nchini Rwanda leo tarehe 21 Juni 2024.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa zoezi hilo, Waziri wa
Ulinzi wa Rwanda Mhe. Juvenal Marizamunda amesema kuwa vikundi vyote
vilivyoshiriki zoezi hilo vimeonesha weledi mkubwa katika nyanja mbalimbali
ikiwemo Ulinzi wa Amani, kukabiliana na majanga ya asili, ugaidi pamoja uharamia.
Naye Kamanda wa vikundi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki
vilivyoshiriki zoezi hilo kutoka JWTZ Brigedia Jenerali Said Hamis Said amesema
kuwa vikundi vimeonesha weledi wa hali ya juu katika kutafsiri na kutekeleza kwa wakati amri na maelekezo
mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika kuwajengea uwezo wa pamoja ili kuviweka
tayari pindi vitakapotakiwa kutoa msaada ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Kikundi cha Tanzania kimeundwa na JWTZ, Polisi, Uhamiaji, Zimamoto
na Uokozi pamoja na Taasisi za Kiraia za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Tukio hilo limehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mheshimiwa Veronica Nduva.



0 Maoni