Bunge la Afrika Kusini lamchangua Ramaphosa kuwa rais

 

Bunge la Afrika Kusini limemchagua Cyril Ramaphosa kuwa rais wa nchi hiyo kufuatia kufikiwa kwa maafikiano ya kuunda muungano baina ya chama cha ANC na vyama vya upinzani.

Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa inaundwa na Chama cha ANC cha Ramaphosa, chama cha mrengo wa kati cha Democratic Alliance (DA) na vyama vingine vidogo.

Katika hotuba yake ya ushindi, Ramaphosa ameupongeza muungano huo mpya na kusema wapiga kura wanataraji viongozi kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya wote na kwa taifa.

Chapisha Maoni

0 Maoni