Spika Tulia na Naibu Waziri Ridhiwani wawatembelea majeruhi wa ajali

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Tulia Ackson na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Ridhiwani Kikwete wamewatembelea majeruhi wa ajali ya gari zilizogongana jana tarehe 29 Machi 2024, mabao wamelazwa katika hospitali ya Msoga.

Ajali hiyo ya gari la abiria aina ya Toyota Coaster iliyokuwa imebeba washabiki wa timu ya Simba waliokuwa wanasafiri toka Mbeya kuelekea Dar es Salaam kuangalia mpira ambapo gari lao lililigonga lori la mizigo likiingia barabarani kutoka kupima uzito kwenye mzani maeneo ya Vigwaza.

Akiongea kabla ya kunkaribisha Spika, Mhe. Kikwete ambaye ni Mbunge wa Chalinze alitoa pole kwa uongozi wa Simba na wafiwa na kuwaombea kwa Mungu majeruhi wapone na warudi salama Mbeya.

Katika kuonyeshwa kuguswa na tukio hilo pamoja na kutenda matendo ya huruma, Mbunge huyo aliamua kulipa gharama za huduma za wagonjwa wote waliohudumiwa hospitalini hapa kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 3.8.

Akizungumza baada ya kumshukuru Mbunge kwa kulipia gharama hizo, Spika wa Bunge Dk. Tulia alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa uliokwisha fanyika hospitalini hapo na kwamba yanayoonekana ni matundo ya uwekezaji huo.

Pamoja na hayo aliwashukuru wote waliojitotea kusaidia pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, na viongozi wa chama kwa niaba wa wote.

Katika msafara huo wa mashabiki wa Simba 27 walijeruhiwa, ambapo wote wameruhusiwa isipokuwa wawili ambao watabaki chini ya uangalizi na wawili walifariki dunia kwa majeraha waliyoyapata katika ajali hiyo.



Chapisha Maoni

0 Maoni