Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya
wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi
amezindua programu ya kugawa taulo za kike (Tumaini Kits) katika viwanja vya
Jadida Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba 29 Machi 2024.
Aidha Programu hiyo inafadhiliwa na Shirika la UNICEF kwa
kushirikiana na Wizara ya Elimu Zanzibar, pamoja na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation
(ZMBF) kwa usambazaji wa Taulo za kike
1000 Unguja na Pemba.
Viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Mhe.Lela Mohamed Mussa, Mkuu wa UNICEF Zanzibar Laxmi Bhawani
na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib.
0 Maoni