Mama anayetuhumiwa kuwanywesha sumu watoto wake wawili na
kuwasababishia vifo mkoani Mbeya, Dainess Paul Mwashambo (30), amefariki dunia
katika hospitali ya mkoa wa Mbeya akipatiwa matibabu.
Taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa leo na Kamanda wa
Polisi SACP Benjamin Kuzaga mtuhumiwa Dainess amefariki dunia Machi 9, 2024
majira ya saa 10:15 jioni wakati akipatiwa matibabu.
Machi 5, 2024 Dainess akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Mashese-
Ilungu aliwanywesha sumu ya kuulia magugu aina ya (Pare Force) watoto wake
wawili na kusababisha vifo vyao na kisha na yeye alikunywa sumu hiyo iliyopelekea
kukimbizwa Hospitali ya mkoa wa Mbeya kwa matibabu.
Taarifa hiyo ya SACP Kuzaga imamalizia kwa kusema kuwa mtuhumiwa
Dainess Paul Mwashambo, aliendelea kupatiwa matibabu Hospitalini hapo lakini tarehe
09 Machi, 2024 alifariki duniani.
0 Maoni