Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameagiza taasisi zinazo husika na sheria kukamilisha
mchakato wa utungaji wa sheria ili kuanza kazi kwa Mahakama Maalum ya Makosa ya
Rushwa na Uhujumu uchumi kwa mwaka huu.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo katika kilele cha Maadhimisho
ya siku ya Sheria Zanzibar katika viwanja vya Mahkama kuu Tunguu, Mkoa wa
Kusini Unguja tarehe 07 Februari 2024.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inaendelea
kuchukua hatua za kuimarisha mhimili wa Mahakama na Taasisi zote za Sheria ili
ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi, hatua hizo ikiwemo ujenzi wa majengo
saba (7) ya Mahkama katika Mikoa na Wilaya Zanzibar, kuongeza idadi ya Majaji,
Mahakimu na Makadhi pamoja na kuboresha maslahi kwa Majaji, Mahakimu, Makadhi
na watumishi wengine wa Taasisi za sheria ili kuongeza ufanisi.
Halikadhalika Rais Dk. Mwinyi amesema ustawi bora wa wananchi utategemea kuwepo kwa misingi imara ya kuheshimu haki za binadamu, utawala bora, uhuru wa Mahakama pamoja na sheria madhubuti zinazoilinda jamii dhidi ya aina zote za unyanyasaji.
Vilevile Rais Dk. Mwinyi ameipongeza Mahakama ya Zanzibar kwa
kuanza mchakato wa kuboresha mfumo wa kieletroniki wa usikilizaji wa mashauri
kwa msaada wa kitalaamu kutoka Mahakama ya Tanzania.
Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amezindua mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahkama (2024-2029) na kukabidhiwa ripoti ya utendaji kazi wa Mahakama ya mwaka 2023.
0 Maoni