Watu wanne wafikishwa mahakamani kwa mauaji

 

Watu wanne wamefikiswa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza na kusomewa shtaka la mauaji ya watu wawili katika kesi namba 2536 ya mwaka huu.

Akisoma shtaka hilo leo Januari 31, 2024 mbela ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo John Jagadi Mwendesha Mashtaka Mkaguzi wa Polisi Juma Kiparo amewataja kwa majina washtakiwa hao kuwa ni Michael Kanzaga ( 19), Malimi Lutema ( 42), Juma Bupilipili ( 32 ) na Kulwa wangale ( 43 ) wote wakazi wa kijiji cha Malemve.

Kiparo ameiambia Mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 11, 2024 huko wilayani Kwimba kwa kumuua Yusuph Mosha (33) mkazi wa Nyamhongoro na Galila Lutobeka (30) Dereva bodaboda na mkazi Nyamhongoro kwa kuwapiga mawe na kuwachoma moto wakiwatuhumu kwa wizi wa kuku kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha Sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo ya mwaka 2022.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka kisheria ya kusikiliza shauri hilo ambapo hakimu ameahirisha shauri hilo hadi tarehe 14.02.2024 itakapotajwa tena.



Chapisha Maoni

0 Maoni