Je, wajua Biblia ya kwanza kuandikwa duniani

 

Biblia ya Ethiopia inaaminika kuwa ndio Biblia ya kwanza kabisa duniani, iliyoandikwa katika ngozi ya mbuzi kwenye karne ya 5.

Biblia hiyo inatambulika kwa jina la Monk Abba Garima, mtu ambaye inasemekana aliandika  maandishi yote ya Biblia hiyo kwa siku moja tu akiwa amejawa na upako.

Biblia ya Garima imefafanuliwa vyema na kuhifadhiwa vizuri. Mfuko wa Urithi wa Ethiopia umetenga fedha kuhifadhi Biblia hiyo.

Biblia hiyo imehifadhiwa kwenye Nyumba ya Watawa ya Garima karibu na mji wa Adwa katika mkoa wa Tigray tangu ilipoandikwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni