Wakuu wote wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa, wametoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja kwa ajili ya kutoa
misaada ya kibinadamu, wakisema kuwa imetosha sasa.
Taarifa hiyo imesema kwa
karibu mwezi moja sasa wamekuwa wakishuhudia hali ya kushangaza na kutisha inayojitokeza
Israel na maeneo ya Palestina, yakupoteza maisha ya watu kadhaa na mpasuko.
Wakuu hao wa UNICEF, WFP
pamoja na Save the Children, wameelezea hali ya kutisha ya vifo vya watu kwa
pande zote mbili, na kutaka kuachiwa huru bila ya masharti mateka wa shambulizi
la Oktoba 7 wanaoshikiliwa na Hamas.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje
ya Marekani amewasili nchini Uturuki, akiendelea na ziara ya Kidiplomasia
katika ukanda huo, na kutaka kusitishwa kwa mapigano.
Awali akiongea akiwa jijini Baghdad,
Antony Blinken alisema kuwa wakuu wa nchi wa ukanda huo wanakaribisha hatua ya
kusitishwa mapigano kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.
Hata hivyo, Israel imesema kwamba
inataka kwanza kuachiwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas kabla ya kufikiwa
hatua ya kusitisha mapigano..
0 Maoni