Tani 8650 za Korosho ghafi
kutoka Chama kikuu cha ushirika RUNALI kinachohudumia wakulima wa Wilaya za
Ruangwa, Nachingwea na Liwale Mkoani Lindi zimeuzwa katika mnada wa tatu wa zao
hilo kwa bei ya juu ya shilingi 2042 na bei ya chini1950.
Mnada huo umefanyika katika
kijiji cha Mkundi kata ya Makata Wilayani Liwale Mkoani Lindi ambapo juma ya
makampuni 31 yamejitokeza kununua korosho hizo.
Akiongea kwenye mnada huo Mrajisi
wa vyama vya ushirika Mkoa wa Lindi Secilia Sothenes amewataka wakulima
kuzingatia ubora wa korosho zao wanazopeleka kwenye maghara.
"Kama tunavyofahamu
sasa ni msimu wa mvua umeshaanza hivyo ni vyema wakulima wakahakikisha wanawahi
kukusanya korosho zao kutoka shambani sambamba na kuzianika vizuri ili zisiende
mnadani zikiwa na unyevu na kupoteza ubora," alisema Sothenes.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika RUNALI amewaahidi wakulima kuendelea kufanya
malipo kwa wakati ambapo amesema kuwa mpaka sasa tayari katika minada miwili
iliyofanya na chama hiko wakulima wameshalipwa fedha zao.
0 Maoni