Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah amefanya mazungumzo na uongozi wa
Kiwanda cha Marumaru cha Keda na kutembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho
kilichopo Chalinze Mkoani Pwani.
Katika mazungumzo hayo
Mkurugenzi Mkuu aliuambia uongozi wa kiwanda hicho kuwa NHC inatembelea viwanda
mbalimbali kuona uwezo, gharama na muda utakaotumika kuzalisha vifaa vya ujenzi
vitakavyosaidia NHC kujenga nyumba za gharama nafuu kwa Watanzania.
Tangu aingie NHC, Hamad
amehimiza kupunguza gharama ya ujenzi wa nyumba kwa kununua vifaa vya ujenzi
moja kwa moja kutoka viwandani ambako bei na ubora wa vifaa hivyo unakubalika
katika kuwezesha ujenzi wa nyumba bora na kwa gharama nafuu.
Uongozi wa kiwanda hicho
umeonyesha nia ya kufanya kazi na NHC katika kuchangia ujenzi wa nyumba bora na
nafuu nchini Tanzania.
Kiwanda hicho kinazalisha
mita za mraba 50,000 za marumaru kwa siku na kinafanya kazi siku 7 za wiki kwa
saa 24. Ziara hii ni muendelezo wa ziara mbalimbali zinazofanywa na NHC katika
viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi.
0 Maoni