KAMISHNA wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) Prof. Dos Santos Silayo amewataka wananchi hususani wanaojishughulisha na
kilimo kuepuka kuchoma moto mashamba na badala yake watumie mbinu mbadala
kufuatia hivi karibuni zaidi ya Hekta 500 za Mashamba ya Miti ya Wananchi Wino
Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kuteketea kwa moto na kujeruhi watu wanne
waliokuwa wakizima moto huo.
Kauli hiyo ameitoa leo baada ya kuwatembelea Majeruhi
watumishi wanne wa TFS waliojeruhiwa na moto katika eneo la Madaba Kijiji Cha
Wino wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Aidha amesema wananchi wanapaswa kujihadhari na uchomaji
moto holela katika maeneo ya mashamba sambamba na kuondoa imani potofu za kuchoma
moto kunaongeza maisha.
Imeelezwa kwamba Shamba la Serikali la Wakala wa Misitu Wino
TFS limeungua kwa sehemu asilimia 0.3

0 Maoni