Nyota wa England Sir Bobby Charlton afariki dunia

 

Nyota wa zamani wa Manchester United, Sir Bobby Charlton, ambaye alitoa mchango kwa England kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1966, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.

Charlton alitwaa makombe 106 kwa England na kufunga magoli 49 katika mechi za kimataifa, na kuweka rekodi kwa taifa lake kwa kipindi hicho.

Katika kipindi chake cha kusakata soka cha miaka 17 akiwa na Manchester United alitwaa makombe matatu ya ligi, Kombe la Europa pamoja na kombe la FA.

Familia ya Charlton, imesema kwamba amefariki akiwa mwenye amani katika majira ya alfajiri siku ya Jumamosi.

Chapisha Maoni

0 Maoni