Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo
Septemba 21, 2023 amefanya ziara ya kukagua ufanisi wa uzalishaji wa maji
Wilaya ya Ubungo na Kinondoni jukumu ambalo linatekelezwa na Mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa
uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji taka ambapo
pesa nyingi zinatumika, na upendo mkubwa alionao kwa wananchi na dhamira yake
ya kumtua ndoo mama kichwani.
Aidha, ameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa Utekelezaji mzuri wa majukumu yao ambapo
kwa sasa DAWASA inauwezo wa kuzalisha Lita milioni 590 kwa siku ikiwa mahitaji
halisi ni Lita milioni 540 " uzalishaji ni hatua moja kubwa na Usambazaji
ni hatua nyingi niwapongeze sana," alisema RC Chalamila.
Vilevile Mhe Albert Chalamila baada kutembelea miradi ya
maji Wazo Wilaya ya Kinondoni na Tegeta A Ubungo amekagua pia mradi wa
Uchakataji maji Mbezi Beach ambao utagharimu zaidi ya Dola milioni 63, amesema
katika Mkoa huo maji taka ni moja kitu kinachosumbua sana hivyo mradi huo ni
mwarobaini wa Changamoto hiyo, amewataka wakandarasi kufanya Kazi hiyo kwa
weledi kukamilisha kwa wakati na kwa Ubora na kuzingatia thamani ya pesa pia ametoa
rai kwa wananchi kutoa ushirikiano katika Kipindi chote cha utekelezaji wa
mradi huo.
Sambamba na hilo Mhe Chalamila ametoa Onyo kwa wadokozi wa
vifaa vya Utekelezaji wa mradi huo yayote atakayebainika hatua za kisheria
zichukuliwe dhidi yake, hata hivyo amewataka wananchi kuwa mabalozi wazuri
katika kutunza vyanzo vya maji na akiwa eneo la shule ya msingi mivumoni
kujioenea Usambazaji wa Maji amewataka walimu kutoa elimu maalum ya kulinda
vyanzo vya maji kwa wanafunzi ili kuwekeza kwenye kizazi hiki cha leo na cha kesho.
Kwa Upande wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Ndg Kiula M.
Kingu amemuahidi Mkuu wa Mkoa kuendelea kuboresha pale panapohitaji maboresho
kwa masilahi mapana ya watu wengi hususani katika utoaji wa huduma ya maji safi
vile vile amesema kukamilika kwa mradi wa kudhibiti maji taka Mbezi Beach
kutaleta faida kubwa ikiwemo Mbolea, Umeme (Biogas) maji na kuondoka kana kwa
kiasi kikubwa na magonjwa ya milipuko hivyo ametoa rai kwa jamii ambayo mradi
unapita kutoa ushirikiano.
Mhe Mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo aliambatana na Kamati ya
usalama ya Mkoa, Viongozi wa Chama ngazi ya Mkoa na wataalam kutoka Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira DAWASA wakiongozwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa
DAWASA Ndg Kiula M Kingu.
0 Maoni