Serikali imelieleza bunge kwamba italifanyia kazi suala la uwezekano
wa biashara kati ya China na Tanzania kufanyika kwa kutumia shilingi ya
Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Jijini Dodoma, kwa niaba ya
Waziri wa Fedha na Mipango, wakati wa kujibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini
Mh. Cosato David Chumi aliyetaka serikali kuwezesha suala hilo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Hamad H. Chande amesema
Serikali italifanyia kazi sula hilo ili kuona nini kinapaswa kufanyika
kuwezesha wafanyabishara wa China kukubali matumizi ya sarafu ya Tanzania.
Hata hivyo, Mh. Chande amesema katika biashara ya kimataifa
wafanyabiashara wanao uhuru wa kutumia sarafu yoyote inayorahisisha biashara na
inayokubalika na nchi nyingine kwa lengo la kupunguza gharama za miamala na
muda.
0 Maoni