Mnyoo mrefu wakutwa hai kwenye ubongo wa mwanamke

Wanasayansi wamesema wamekuta mnyoo wenye urefu wa sentimita 8 ukiwa hai kwenye ubongo wa mwanamke raia wa Australia.

Wanasayansi wamesema tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea duniani, na kuongeza kwamba huenda mnyoo huo mwekundu ulikuwapo kwenye ubongo kwa muda wa miezi miwili.

Mnyoo huo ulitolewa kwenye upasuaji kwa mgonjwa huyo aliyezaliwa Uingereza, na ulikuwa umeathiri mishipa mwembamba ya mbele ya ubongo.

Watafiti wameonya kwamba tukio hilo lionaonyesha hatari iliyopo ya kupata maambukizi yanayosambaa kutoka kwa wanyama.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni