Wanachi nchini wameimizwa kuwaenzi Mashujaa wa Vita vya Majimaji kwa kudumisha Umoja, Mshikamano, Upendo na Uzalendo kama walivyoishi Mashujaa waliopigania Utu na heshma ya watu wote.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.
Christopher Ngubiagai kwaniaba ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary
Masanja, katika Tamasha la Vita vya Majimaji Nandete Kilwa Mkoani Lindi,
Vilivyoanzoanzia Nandete Mwaka 1905.
Mhe. Ngubiagai ameongeza kuwa Vita waliopigana Mashujaa wa
Vita vya Majimaji dhidi ya Ukoloni, viendelee kuhamasisha na kuongeza nguvu
katika Vita dhidi ya Umasikini, watu kufanya kazi Kwa bidii na kwa uwanifu ili
nchi hizidi kuinuka kiuchumi.
"Wapiganaji wa vita hivi hawakuwa na silaa za moto bali
silaa kubwa walizotumia ni Mshikamano na Upendo usiopimika kwa ajili ya kizazi
kilichopita na kizazi hiki, hivyo tuzitumie silaa hizi za Mashujaa wetu katika
kuipenda nchi yetu na kudumisha Utamaduni wetu" Mhe. Ngubiagai
Akizungumza kwenye Tamasha hilo, Chifu wa Wamwera Chifu
Nakotyo Malibiche Ilulu amesisitiza jamii kudumisha Utamaduni na kuzingatia
maadili mema, kupambana na Mmomonyoko wa Maadili unaotokana na vijana kuiga
tamaduni za nje zisizofaa.
Naye Chifu wa Kabila la Kimatumbi Mkoa wa Lindi, Mkulungwa
Mkulungwa Mbonde Shukuru Mungu ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
kuunga Mkono juhudi za Wamatumbi katika uwanzishwaji na undelezwaji wa Tamasha la
Vita vya Majimaji jambo linalopelekea wananchi kunufaika na maendeleo
mbalimbali hususani ya maboresho ya Miundombinu kama vile barabara.
Na Sixmund Begashe
0 Maoni