Pape Sakho aachana na Simba, atimkia Ufaransa

 

Klabu ya Soka wekundu wa Msimbazi Simba SC imempa mkono wa kwaheri mchezaji wake kiungo mshambuliaji Pape  Sakho 


Katika taarifa yake imeachana na mchezaji huyo baada ya kununuliwa nchini Ufaransa “tumefikia makubaliano na klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) ya nchini Ufaransa kumnunua mchezaji wetu Pape Sakho.


Tunamtakia kila la kheri Sakho kwenye timu yake mpya. 


Sakho atakumbukwa katika historia baada ya CAF kuchagua  bao bora la kwanza la Sakho dhidi ya Asec Mimosas huku jingine ambalo limeshika nafasi ya nne ni lile alilolifunga kwa Mkapa dhidi ya RS Barkane 

Chapisha Maoni

0 Maoni