Beyonce achangia ongezeko la mfumuko wa bei Sweden

 

Unafikiri vita ya Ukraine imechangia kuongeza gharama za maisha?, huenda hufahamu  kuhusu mwanamuziki Beyounce, ambaye sasa analaumiwa kwa kuongeza gharama za maisha nchini Sweden.

Kuanza kwa (World Tours) ziara ya dunia ya mwanamuziki huyo Sweden mwezi uliopita kumechangia ongezeko la wateja mahotelini na bei za vyakula hotelini, takwimu za uchumi za nchi hiyo zimeonyesha.

Nchi ya Sweden imeshuhudia ongezeko la mfumuko wa bei uliofikia asilimia 9.7 mwezi Mei, huku ongezeko la bei za hoteli kwa malazi na chakula zikitajwa kuchangia kupanda kwa mfumuko huo wa bei.

Mchumi Michael Grahn wa Danske Bank, amesema kwamba anadhani kwamba ziara ya muziki ya Beyounce imechangia kupanda kwa gharama za malazi na vyakula kwenye hoteli nchini humo kutokana na ongezeko la wageni.

Chapisha Maoni

0 Maoni