Msigwa afafanua madai bandari ya Dar es Salaam kuuzwa miaka 100


Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa ametoa ufafanuzi kuhusiana  sakata la madai ya bandari ya Dar es Salaam kuuzwa miaka 100 kwa Dubai.

Akitoela ufafanuzi kuhusu mjadala huo ambao umekuwa mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu azma ya serikali kutaka kuingia makubaliano ya kuipa kandarasi kampuni ya DP World kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu kusimamia bandari hiyo.



Kwa mujibu wa Msingwa akizungumza na Wasafi Fm , ameeleza  kuwa makubaliano ya awali ya kushirikisha kati ya pande hizo mbili ndio yamesainiwa lakini sio mkataba wa miaka 100 kama unavyoelezwa na kuwa bado hakujatiwa saini ya mwisho kuhusu vipengele vya namna gani makubaliano hayo yatafanyika.



Amesema kuwa makubaliano yaliyofanyika yanadumu kwa miezi 12 “baada ya makubaliano hayo kama kutakuwa kunakuelewana ndipo mnakwenda sasa kwenye mikataba ya utekelezaji na ndiyo itakuwa inaeleza namna ambavyo uendelezaji utakavyofanyika” 


Kwa mujibu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho, alibainisha bandari  ya Dar es Salaam ndio kuu nchini Tanzania, haitoi huduma kwa Tanzania pekee. Nchi jirani zisizo na bahari zinatumia bandari hiyo vilevile; Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda na Zimbabwe.


“Watumiaji wa bandari ya Dar es Salaam, wameongezeka sana, kwa sasa ndani ya mwaka mmoja tunahudumia magari kati ya 250,000 hadi 300,000 na asilimia 60 ya magari hayo, ni ya nchi jirani,”

Chapisha Maoni

0 Maoni