Rais Mstaafu Kikwete akutana na washindi riadha

 

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Wanariadha Gabriel Geay na Wence Tarimo walioshiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023. 


Gabriel Geay aliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo. Mheshimiwa Rais Mstaafu amempongeza Gabriel Geay kwa ushindi mkubwa na kwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. 

Pamoja na wanariadha hao, walikuwepo pia wahamasishaji mbalimbali akiwemo “Bongo Zozo”. Amewapongeza pia kwa kuhamasisha ushindi huu na kufanikisha kuinua bendera ya Tanzania juu. 


Mheshimiwa Rais Mstaafu yuko Boston, Marekani ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Harvard “Harvard Ministerial Leadership Program”. Katika mafunzo hayo, Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Fedha wa Zanzibar ameshiriki pia.


Chanzo: Hakingowi

Chapisha Maoni

0 Maoni