Maazimio
hayo yamepitishwa katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu kilichoongozwa na
Mwenyekiti wa UVCCM, Mohammed Ali Kawaida, kilichofanyika katika Ukumbi wa NEC,
Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Baraza pia
limeipongeza Serikali ya Rais Samia kwa utekelezaji wa miradi ya kimkakati,
kuimarisha uchumi, diplomasia ya kimataifa pamoja na kuboresha huduma za afya
na kijamii.
Aidha,
limempongeza Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa juhudi zake za kuimarisha
maridhiano ya kisiasa visiwani Zanzibar.
Katika
azimio la pili, Baraza Kuu la UVCCM limekemea kwa kauli moja vitendo vya
uchochezi wa vurugu na uvunjifu wa amani vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya
wanasiasa na wanaharakati, likisisitiza kuwa halitasita kusimama mstari wa
mbele kupinga mtu au kikundi chochote kitakachohatarisha amani na utulivu wa
Tanzania.

0 Maoni