Tanzania na Urusi zina uhusiano wa kihistoria wenye
hekima, heshima na ushirikiano wa pande mbili unaoheshimiana. Tofauti
na nchi za Magharibi ambazo zilitumia ukoloni, unyonyaji na utumwa
kuwatawala Waafrika kwa karne nyingi, Urusi haijawahi kuwa na koloni.
Badala yake, imekuwa mshirika wa dhati katika mapambano yetu ya uhuru
na maendeleo.
Tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, Umoja wa Kisovyeti uliunga mkono kwa dhati
harakati za uhuru wa Tanganyika na Zanzibar. Walitoa misaada ya
kielimu, kijeshi na kiuchumi kwa harakati za ukombozi barani Afrika.
Maelfu ya vijana wa Tanzania walisoma katika vyuo vya Urusi na kurudi
nyumbani na elimu bora.
Wakati wa Vita vya Kagera (1978-1979),
Urusi iliunga mkono Tanzania kwa kusimama upande wa haki na kupunguza
msaada kwa dikteta Idi Amin aliyevamia nchi yetu.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,
ameanza ziara rasmi ya kihistoria nchini Urusi kuanzia leo Juni 3,
2026.
Hii ni ziara ya pili ya Rais wa Tanzania nchini Urusi
katika historia ya nchi yetu. Ziara ya kwanza ilifanyika mwaka 1969
wakati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipaalikwa rasmi na viongozi
wa Umoja wa Kisovyeti. Baada ya miaka 57, Rais Samia anafuata nyayo
za Baba wa Taifa katika kuimarisha uhusiano huu muhimu.
Ziara
hii inatarajiwa kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara,
nishati, madini, elimu, sayansi na teknolojia. Rais Samia anakutana
na Rais Vladimir Putin Kremlin na kushiriki katika St. Petersburg
International Economic Forum.
Kwa Watanzania, Hii ni fursa ya
kutambua na kuthamini marafiki wetu wa kweli. Urusi inaheshimu uhuru
wetu na inataka ushirikiano wa pande mbili bila masharti ya kisiasa.
Tuunge mkono ziara hii ili ilete matunda halisi kwa maendeleo ya
Tanzania yetu.

0 Maoni