Na. Beda Msimbe, TBN, Moscow
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Vnukovo, uliopo Jijini Moscow kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa, nchini
Urusi
Katika ziara hii ya kihistoria ikifanywa kwa mara ya
pili katika historia ya uhusiano wa Tanzania na Urusi, ya kwanza
ilikuwa ni miaka ya 1960 iliyofanywa na baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere, Rais Samia anaendeleza kampeni kubwa ya kuhakikisha Tanzania
inanufaika pia kiuchumi na uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali
Kwa mujibu wa shughuli atakazofanya Rais Samia akiwa hapa nchini kwa
lengo la kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi na
kihistoria baina ya Tanzania na Urusi,Rais amekuja kuiweka Tanzania
katika ramani ya uwekezaji kwa ushiriki wake katika mkutano mkubwa wa
uwekezaji jijini St Petersburg na pia kuona namna ya kutengeneza
raslimali watu ambayo taifa inahitaji sana katika kufanikisha
utekelezaji wa dira ya maendeleo ya 2050.
Alipowasili nchini
hapa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo, Jijini Moscow
majira ya saa mbili na dakika 25 usiku , japo jua bado lilikuwa
linawaka, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokea heshima ya wimbo wa
Taifa pamoja na gwaride.
Rais Samia alipokewa uwanjani na
Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi Mhe. Maxim
Reshetnikov.
Kwa mujibu wa ratiba leo asubuhi ataanza na
kuweka shada ka maua kwa kaburila askari asiyejulikana kabla ya
kwenda Ikuku ya Kremlin kwa mazungumzo na Rais Vladmir Putin.


0 Maoni