Wakati
majirani na 'mawakala' wa uongo wakikesha kusambaza propaganda kuwa Bandari ya
Dar es Salaam ina kulegalega, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Jemedari Dkt. Samia
Suluhu Hassan imewajibu kwa vitendo kwa kuandika historia nyingine ya dhahabu.
Safari
hii, si meli ya kawaida, bali ni chuma cha kisasa, Höegh Australis, meli
inayotumia nishati safi ya gesi asilia (LNG), imetia nanga katika maji ya
Tanzania na "kuelea" kwa mbwembwe ikiwa imesheheni magari 1,006, huku
ikithibitisha kuwa Dar es Salaam sasa ndiyo mtembezi wa anga za kimataifa.
Ujio
wa meli hii yenye urefu wa meta 200 kutoka kampuni ya Höegh Autoliners
(Norway), ni salamu tosha kwa wale waliozoea kudhani Tanzania bado ipo kwenye
zama za kale. Huu ni ushahidi kuwa maboresho ya miundombinu si maneno ya
majukwaani, bali ni hali halisi inayovutia miamba ya usafirishaji duniani.
Kwa
ujio wa meli hii Tanzania imeingia kwenye ramani ya dunia kwa kupokea meli zinazotumia
nishati rafiki (LNG), jambo ambalo nchi nyingi jirani bado zinaliota.
“Bandari
ya Dar es Salaam sasa ni lango la kimataifa, si la kikanda tu. Maboresho ya
miundombinu, matumizi ya teknolojia na huduma za kisasa vimeivutia meli kubwa
kama hii,” alisema Prosper Setebe, wakala wa meli hiyo kutoka kampuni ya EACS.
Majibu
kwa "Wabishi" na Propagandista
Kwa
muda mrefu, kumekuwa na kelele za hapa na pale zikijaribu kupaka matope ufanisi
wa bandari yetu. Lakini Höegh Australis imekuja kama "pingu" ya kufunga
midomo hiyo. Meli hiyo ilihudumiwa fasta na kuondoka bandarini katika muda
zaidi ya sahihi.
"Ufanisi
huu kwenye kasi ya kushusha na kupakia mizigo unatokana na mfumo kwenda
"ki-digitali".
Aidha
meli hii kubwa na nyingine ambazo ni za kimkakati haziwezi kutia nanga kwenye
bandari isiyo na usalama na amani ya kudumu, ujio wao ni kudhihirisha kuwa
Tanzania ipo tulivu na inaendelea kujenga uchumi wake.
Maboresho
haya ni matokeo ya utulivu wa kisiasa na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
ambaye amefungua milango ya uwekezaji. Wakati wengine wakishangaa meli
zinazopita, Tanzania inashangiliwa kwa kuleta meli za kisasa zinazobeba uchumi
wa mataifa mengi.
Wakala
Setebe ametoa wito kwa wadau wa ndani na nje: "Njooni Dar es Salaam, huku
ndipo kwenye ufanisi, huku ndipo kwenye kasi!"
Huku
kukiwa na maoni ya hapa na pale mitandaoni, baadhi wakijaribu kupunguza ukubwa
wa jambo hili, ukweli unabaki palepale; Tanzania si nchi ya mchezo mchezo.
Tumeshawazidi majirani kwa hatua za kiufundi, miundombinu, na uaminifu wa kimataifa.
Kama
walitegemea kuona bandari inafungwa, wameambulia kuona meli kubwa zaidi
zikiingia. Hii ni Tanzania ya kazi, utulivu, na maendeleo ya kweli.

0 Maoni