Jeshi la Polisi Tanzania limesema limeanza kufanyia
kazi taarifa za madai kuwa aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey
Polepole ametekwa ili kubaini ukweli wake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 6, 2025
na Jeshi la Polisi, imesema limeona taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya
kijamii kutoka kwa baadhi ya ndugu wa Polepole wakidai kuwa ametekwa.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limesema linaendelea
kumsubiri, Humphrey Polepole, kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai ili kutoa maelezo kuhusu tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia
mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, Polepole
alitumiwa barua ya wito kwa mujibu wa sheria, lakini hadi sasa hajajitokeza
kama alivyotakiwa kufanya.


0 Maoni