Maonesho ya Tourism Road Show yaliyoanza tarehe 6
Okoba, 2025 nchini Hispania yamemalizika
leo tarehe 8 Oktoba, 2025 katika jiji la
Seville, yakihitimisha ziara ya siku tatu iliyofanyika katika majiji ya
Barcelona, Madrid na Seville kwa kukutana na mawakala wakubwa wa Utalii kwa
lengo la kudani vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji.
Maonesho hayo yaliyowakutanisha mawakala wa safari
za kitalii takribani 100 kutoka Hispania yametoa fursa kwa Tanzania kupitia
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
kuendelea kushika Soko la utalii barani Ulaya ambapo ni soko la kimkakati.
Mkurugenzi wa chama cha wakala wa usafiri Hispania
Bw. Oscar Gabaldòn ambaye pia ni
mwakilishi wa Tanganyika expedition nchini hapo, alisema kwamba lengo la
kuandaa road show hiyo ni kutokana na
mwamko wa watalii nchini hapo kupendelea kutembelea vivutio mbalimbali
vilivyopo Tanzania.
“Tanzania ni nchi yenye uzuri wa kipekee ambayo
imebarikiwa vivutio vya wanyamapori, utamaduni, fukwe nzuri, Milima ya kuvutia
ambavyo nyote hivi vinafanya urahisi kwenye Soko la utalii hapa nchini na ndani
ya bara la ulaya kwa ujumla,” alisema Oscar.
Kwa upande wa washiriki kutoka Ngorongoro na TANAPA
wameleza kuwa kupitia maonesho hayo wamepata fursa ya kuuza vivutio vya Utalii
pamoja na fursa za uwekezaji zilizo ndani ya maeneo yanayosimamiwa na taasisi
hizo kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii nchini na kuwezesha kufikia lengo
la taifa la watalii milioni nane (8)
ifikapo mwaka 2030.



0 Maoni