Katika kipindi hiki
muhimu sana kinachoelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 29 Oktoba, kumetokea kauli kali,
za uchochezi, na zenye kutaka kuvuruga amani kupitia mitandao ya kijamii,
zikijaribu kushawishi wananchi kukata tamaa na kutumia njia zisizo za kikatiba.
Kufuatia matamko hayo
yanayolenga kuingiza taifa katika machafuko, viongozi wa kitaifa, wadau wa
amani, na vyombo vya habari vimekuwa vikitoa wito wa dharura: Wajibu wa Kulinda
Amani ya Taifa uko mikononi mwa kila Mtanzania!
Amani Kwanza,
Mustakabali Kwanza
Wakati tunatambua
kuna hisia za kutoridhika na mchakato wa uchaguzi kwa baadhi ya wananchi,
tunasisitiza kuwa suluhisho la changamoto za kisiasa halipatikani kwenye
vurugu, machafuko, au ‘uwenda wazimu wa halaiki,’ bali kwenye utulivu na
busara.
"Amani yetu ni
urithi tuliopewa, hatuwezi kuutupa kwa ajili ya hisia za muda mfupi. Uchaguzi
ni mustakabali wa nchi yetu. Tunawahimiza wananchi wote, bila kujali hisia zao,
kuonyesha ukomavu kwa kufanya maamuzi yenye tija na kwenda kupiga kura kwa
amani," anasema Mchambuzi wa Siasa na Amani Vivian Gabriel.
Sanduku la Kura Ndiye
Hakimu Mkuu
Hoja ya kwamba
uchaguzi unakosa maana au kwamba kura haina nguvu, inapingana na misingi ya
demokrasia yenyewe. Mabadiliko ya kweli huanzia kwenye uamuzi wa kila mwananchi
katika kituo cha kupigia kura.
Nini Wajibu Wako?
Piga Kura, Kataa
Machafuko: Kura ndiyo njia pekee ya kisheria na kikatiba ya kuweka viongozi
wanaowajibika. Kukataa kupiga kura, au kufuata wito wa kuingia kwenye fujo, ni
kujisalimisha kwa watu wanaotaka kuona nchi ikiingia katika mgogoro.
Thamini Busara: Baada
ya uchaguzi, bila kujali matokeo, nchi nzima itahitaji utulivu ili kujitathmini
na kuendelea kujenga. Machafuko hayataleta ripoti unayotaka wala hayataleta
dawa hospitalini. Yataleta maafa ambayo yatazuia maendeleo kwa miaka mingi.
Kataa Vurugu za
Mitaani: Wito wa "kutukutana barabara kuu" ni mtego wa kutaka
kuingiza taifa kwenye machafuko. Amani ya nchi ni ya thamani kuliko malengo ya
kisiasa ya mtu binafsi au kikundi chochote. Njia sahihi ya kuonyesha
kutokukubali inapaswa kufuata utaratibu wa kisheria.
Katika mahojiano
mbalimbali Vyombo vya usalama vimehimizwa kuchukua hatua kali dhidi ya mtu
yeyote anayeeneza ujumbe unaokusudia kuvuruga amani na utulivu. Tanzania lazima
iendelee kuwa kisiwa cha amani.
Tarehe 29 Oktoba ni
siku ya kutekeleza wajibu wa Kikatiba, si Siku ya Kuteketeza Taifa!
Wananchi popote
walipo iwe Bunju, Kariakoo, Temeke, Mbagala, na maeneo mengine yote nchini
kutafakari kwa kina na kuchagua amani. Nenda kapige kura, onyesha ukomavu wa
kisiasa, na epusha nchi kuingia katika machafuko.

0 Maoni