MGOMBEA mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi amehitimisha mikutano yake ya
hadhara ya kampeni katika Mkoa wa Tabora huku akiacha ujumbe kuwa ifikapo
Oktoba 29 mwaka huu wananchi wa mkoa huo wampigie kura mgombea urais wa Chama
hicho Dk. Samia Suluhu Hassan.
Dk.Nchimbi amehitisha ziara leo Oktoba 6, 2025 katika Mkoa wa Tabora ambapo katika mikutano
ya kampeni mbali ya kumuombea kura mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassan,
wabunge na madiwani pia ametumia mikutano hiyo kunadi sera na Ilani ya uchaguzi
mkuu ambayo imelenga kuleta maendeleo ya watanzania.
Akiwa katika mkutano wa kampeni Dk.Nchimbi kabla ya
kuanza kuwahutubia Wananchi amesimikwa kuwa msaidizi wa Mtemi, kimila akiitwa
'MTONGI' baada ya mkubwa wake Chifu
Hangaya ambaye ni Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Nchimbi amesimikwa na viongozi wa kimila wa
Unyanyembe (Tabora) kwenye mkutano wake wa mwisho wa kampeni mkoani humo,katika
kata ya Kigwa jimbo la Igalula, wilaya ya Uyui nakupewa jina la "NYUNGU YA
MAWE".
Pamoja na mambo mengine,Dkt.Nchimbi aliwanadi
wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Igalula, Ndugu
Juma Ramadhan Mustafa [KAWAMBA) pamoja na Madiwani.
Aidha Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwaomba
wampigie kura za ushindi wa kishindo
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,Dkt.Samia Suluhu
Hassan,Wagombea Ubunge na Madiwani kwa ujumla.
Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 18 sasa tangu
kuzinduliwa kwa kampeni hizo Oktoba 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea
kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.




0 Maoni