CPA Musa
Kuji, Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) leo
Oktoba 1, 2025 amefungua rasmi kikao kazi cha maafisa rasilimali watu na
utawala ndani ya taasisi mama ya uhifadhi.
Kikao kazi hicho kilifanyika jijini Arusha kwa
lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi na kuandaa
mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo ili Maafisa na Askari Uhifadhi wa
TANAPA waweze kufanya kazi kwa ari na ufanisi ili Shirika liweze kufikia
malengo yake.
Kikao
hicho pia, kilihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Shirika - Kamishna
Msaidizi wa Uhifadhi Abdallah Kiwango, Mkuu wa Sehemu ya Utawala - Kamishna
Msaidizi wa Uhifadhi Peter Butiku, pamoja na Mkuu wa Sehemu ya Utumishi na
Rasilimali Watu - Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Cecilia Mtanga.
Ifahamike
kuwa Idara ya Utumishi na Rasilimali Watu ni muhimu hasa katika kuhakikisha
kuwa rasilimali ya adimu yenye vipawa na weledi tofauti (watumishi) wanakuwa na
mazingira bora na wezeshi ya kutekeleza majukumu yao pasina mawaa.



0 Maoni