Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi
Maalum kupitia Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwa kushirikiana na
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, imefanya ufuatiliaji wa mashirika yasiyo
ya kiserikali yanayotekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Mashirika yaliyotembelewa ni pamoja na TAWREF na KIVUCE
yanayotekeleza shughuli zake katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, YEPAO na
Courage World Wide yanayotekeleza miradi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya
Moshi, huku wilayani Hai ni VOEWOFO na
Kilimanjaro New Vision Sober House pamoja na DSW & HRNS inayopatikana
wilayani Siha.
Akizungumza kuhusu lengo la ufuatiliaji huo, Wakili kutoka
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Tatu Ally, alisema kuwa hatua hiyo inalenga,
Kusaidia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs)
yanayotekeleza afua kwa makundi yaliyo hatarini, hususan wasichana balehe na
wanawake vijana, kuhakikisha yanazingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya uratibu
wa NGOs nchini.
Pamoja na Kubaini changamoto na mapungufu katika utekelezaji
wa miradi ili kutoa ushauri na kutafuta suluhisho sahihi na Kufuatilia matokeo
ya miradi ili kuhakikisha afua zinazotekelezwa zina manufaa kwa jamii na
kubaini maeneo yanayohitaji maboresho.
Vile vile Kuyajengea uwezo mashirika hayo kupitia mafunzo ya
Mfumo wa Uratibu wa NGOs (NIS), Mwongozo wa Uratibu pamoja na Mkakati wa Taifa
wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NSNS) 2022/2023 – 2026/2027.
Aidha, ufuatiliaji huu ni sehemu ya jitihada za Serikali
kuhakikisha mashirika yasiyo ya kiserikali yanaendelea kutekeleza majukumu yake
kwa ufanisi, uwazi na kwa manufaa ya jamii hususan makundi yaliyo katika
mazingira hatarishi.
0 Maoni