Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa tiketi 10000 zenye
thamani ya Shilingi Milioni 20 kwa ajili ya mashabiki kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu ya Tanzania (Taifa Stars),
itakayokabiliana na Burkina Faso katika mchezo wa kwanza wa Mashindano ya CHAN
2024 leo Agosti 02, 2025.
Hayo yameelezwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa
Serikali, Ndg. Gerson Msigwa wakati akiwasilisha fedha hizo kwa kampuni ya N
Card ambapo mashabiki watakaowahi watakabidhiwa.
0 Maoni