Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Mluya, ameahidi kwamba ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani atahakikisha anafuta kikokotoo cha mafao ya wastaafu ili kuboresha maisha ya wastaafu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili kutoka Dodoma, mgombea huyo amesema pia atahakikisha mtumishi wa umma aliyefanyakazi mwaka mmoja bila kupatwa na kosa lolote anakopeshwa nyumba.
Pamoja na mambo mengine mgombea huyo amesema, amejipanga kushughulikia changamoto mbalimbali, ikiwemo za sekta ya afya ambapo amesema anakwenda kukomesha tabia ya hospitali kuzuia maiti.
“Sasa hivi wafiwa huwa wanamisiba miwili, wa kufiwa na wa gharama za matibabu wanazorundikiwa baada ya ndugu yao kufariki, sisi DP tunakwenda kukomesha tabia hiyo ili kuwapunguzia machungu wafiwa,” alisema Bw. Mluya.
0 Maoni