WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Agosti 30, 2025
amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa matumizi ya
Nishati Safi ya Kupikia katika Magereza 129 nchini.
Uzinduzi huo umefanyika katika gereza la Karanga lililopo
Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa niaba ya magereza yote nchini.
Mpaka sasa vyanzo vya nishati mbadala vinayotumika katika
magereza ni Gesi Vunde (BIOGAS), Mkaa Mbadala (Briquettes), Kuni Poa na Gesi
Asilia (NATURAL GAS) na umeme.
Mheshimiwa Majaliwa amesema hatua hiyo ni ya kupongeza kwa
kuwa inaunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha jamii yote inatumia
nishati hiyo na hivyo kwa kiasi kikubwa kuondoa madhara yatokanayo na matumizi
ya nishati isiyo safi.
Akizungumza wakati akitoa taarifa ya mradi huo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Msimamizi wa Kitengo cha Kilimo, Mifugo na Utunzaji wa Mazingira kutoka Jeshi la Magereza SACP Daimu Mmolosha amesema lengo la jeshi hilo ni kuhakikisha kunakuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha nishati ili kuepukana na matumizi ya kuni ma mkaa.
0 Maoni