Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Agosti
11, 2025 ameshiriki mazishi ya Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Hayati Job Yustino Ndugai yaliyofanyika katika Kijiji cha Sujulile,
wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma.
Mazishi hayo yameongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi pamoja na
Viongozi wa Dini.
0 Maoni