Mfuko wa Mawasiliano kwa
Wote (UCSAF) umeendelea kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo ya vijijini
waliofikiwa na huduma za mawasiliano kupitia minara 758 inayojengwa kwa ruzuku
ya Serikali. Ujenzi wa minara hii unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini na
umefikia asilimia 78.63 ya utekelezaji wake.
Kampeni hii inalenga
kuwafahamisha wananchi kuwa, ujenzi wa minara ya mawasiliano katika maeneo ya
vijijini unatekelezwa kwa ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia UCSAF.
Ruzuku hii inalenga
kuhakikisha wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa
wawekezaji wa sekta binafsi, wanapata huduma za mawasiliano bila kuathiriwa na
changamoto za kijiografia au umbali wa maeneo yao.
Wananchi waliopatiwa elimu hii wamesema, huduma za mawasiliano zimeleta mabadiliko katika maisha yao ya kila siku, hasa katika nyanja za kijamii, kiuchumi, na kielimu. Aidha, wamepongeza juhudi za UCSAF kwa kuwaelimisha kuhusu mchango wa Serikali katika kuwafikishia huduma hizi, jambo ambalo limeongeza uelewa wao na ushiriki katika shughuli za maendeleo ya taifa.
#MawasilianoKwaWote #Minara758NchiNzima
#DigitallyInclusiveTanzania #DigitalEconomy
0 Maoni