Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Kampuni ya Vodacom imeanza kutoa huduma ya matibabu bila malipo kwa wakazi wa mkoa wa Tanga na maeneo ya jirani.
Huduma hizo zinatolewa
katika viwanja vya Chuo cha Ualimu
Korogwe kuanzia Julai 21 hadi 23 2025 baada ya hapo timu hiyo itahamia mkoani
Kilimanjaro.
Huduma zinazotolewa katika
kambi hiyo ni pamoja na uchunguzi na matibabu ya macho, afya ya kinywa na meno,
magonjwa ya akina mama na afya ya uzazi, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya afya ya
akili, sukari na homoni, huduma za maabara, matumizi sahihi ya dawa pamoja na
saratani ikiwemo tezi dume.
0 Maoni