Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza zoezi la
kupasha misuli (warm up), baadaye kuzindua rasmi na kuongoza mbio za Great
Ruaha Marathon leo Julai 05, 2025
Ibuguziwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha huku zikibeba Kauli Mbiu;
“Tuko Tayari Kuvibe na Kutalii.”
Akizungumza katika
tukio hilo, Mheshimiwa Majaliwa ameto wito kwa waratibu wa mbio hizo kuweka
mikakati ya kuzifanya ziwe za kimataifa ili ziweze kukutanisha raia wa mataifa
mbalimbali duniani.
Lengo la Mbio hizo ni
kuhamasisha uhifadhi wa mazingira wa Mto
Ruaha Mkuu ambao ni uti wa mgongo wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kuifanya
jamii kuona umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na kuhimiza matumizi endelevu ya
rasilimali za asili.
Mbio hizo pia
zimehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James viongozi waandamizi wa
Mkoa na wilaya zake, Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Musa Nassoro Kuji na viongozi
waandamizi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
0 Maoni