Ngoma za asili, kwaya
na Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flavor) ni sehemu ya fani ambazo zimekuwa
zikishindaniwa katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa
shule za Msingi na Sekondari (UMITASHUMTA & UMISSETA).
Mratibu wa michezo-
TAMISEMI, Yusuph Singo amesema kupitia sanaa, wanafunzi wanapata nafasi ya
kuonesha vipaji vyao katika kucheza ngoma zenye asili ya makabila ya mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, kuimba nyimbo zenye ujumbe wa
kizalendo na kuburudisha kupitia muziki wa kizazi kipya.
Mikoa inayoshiriki
UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 Mkoani Iringa inatarajiwa kuwa na uwakilishi wa
vikundi vya ngoma, kwaya na waimbaji wa muziki wa kizazi kipya kwa ajili ya
kushindana na kumpa mshindi wa mashindano ya mwaka huu.
Mashindano hayo yenye
kauli mbiu isemayo "Viongozi bora ni msingi wa maendeleo ya Taaluma, Sanaa na Michezo, Shiriki
Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu" yataanza Mei 7 2025 na yanatarajiwa
kufunguliwa rasmi Mjini Iringa tarehe 9 Mei 2025 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
Ofisi ya
Rais-TAMISEMI ndio mratibu na msimamizi wa UMITASHUMTA & UMISSETA 2025
ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, na Wizara ya Habari
Sanaa Utamaduni na Michezo.
0 Maoni