Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka
Zanzibar na kuwasili nchini Zimbabwe kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Rais Dkt. Mwinyi,
akiambatana na Mkewe, Mhe. Mama Mariam Mwinyi, alipokelewa katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, jijini Harare, na Balozi wa
Tanzania nchini humo, Balozi CP Suzan Kaganda.
Rais Dkt. Mwinyi
anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, katika mkutano huo ambao utajadili Mwongozo na Uhifadhi Endelevu wa
Biashara ya Kaboni katika nchi wanachama wa SADC.
0 Maoni