Kampuni ya viatu ya Japan ya
Potato Limited imeuteka ulimwengu viatu kwa ubunifu wa raba yake inayojulikana
sokoni kwa chapa ya Tokyo Kimono Shoes
inayouzwa dola za Marekani 325.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Shotaro Kawamura anatengeneza raba hizo kwa kutumia kitambaa
cha vazi la utambulisho wa kitamaduni Japan la kimono, ambalo huvaliwa mara
chache siku hizi.
Kwa kawaida vazi hilo hutumika tu
katika hafla rasmi, na mara nyingi huhifadhiwa kwa vizazi, na wachambuzi wanadhani
kuwa kuna mabilioni ya dola ya thamani ya mavazi ya kimono yaliyohifadhiwa na yasiyotumika
katika makabati ya Wajapani.
“Kwa
kubadilisha muundo ili tuweze kutumia vitambaa vya kimono katika maisha ya kila
siku, tunaweza kuhifadhi utamaduni kwa njia tofauti,” alisema Kawamura.
Je, umeshawahi kufikiria kuwa unaweza
kununua jozi moja ya raba kwa dola 325 ambayo ni sawa na karibu shilingi
870,000 za Tanzania.
0 Maoni